Ligi Kuu

Ndanda kujipima na Namungo fc!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Ndanda fc itakua na mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya majirani zao  Namungo fc ili kujiweka tayari na urejeo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuruhusiwa kuendelea kuchezwa kama kawaida na serikali.

Mchezo huo utapigwa katika dimba la Nang’wanda Sijaona mkoani Mtwara majira ya saa kumi jioni siku ya Jumamosi. Mashabiki wa Ndanda wamekua na hamu ya kuiona timu yao, hivyo Jumamosi watajitokeza kwa wingi kuitazama timu yao baada ya siku zaidi ya 75 kupita.

Ndanda fc na Namungo walipokutana katika mchezo wakwanza wa Ligi.

Vilabu vyote hivi viwili vinapatikana Mikoa ya Kusini mwa Tanzania Ndanda fc (Mtwara) na Namungo fc (Lindi).

Klabu ya Ndanda inashika nafasi ya 16 katika msimamo ikiwa na alama 31. Kwa alama hizo na nafasi yao Ndanda ipo katika hatari ya zaidi ya kushuka daraja. Kwa upande wa Namungo fc wao wanashika nafasi ya nne wakiwa na alama 50 huku wakiwa wameshuka dimbani mara 28.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.