Mataifa Afrika

Ni heshima kubwa kuitwa na Amunike – Miraj

Sambaza....


Miraj Athuman, jezi namba 7 miongoni mwa namba maarufu duniani, ndiyo anayoivaa akiwa katika klabu yake ya Lipuli Fc. Msimu huu umekuwa mzuri sana kwa Miraj, katika Ligi kuu, Kuitwa timu ya taifa na sasa kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho, ASFC.

Kandanda ilimtafuta na kupata mawili matatu kutoka kwa winga wa kulia huyu mtukutu uwanjani na mcheshi wakati wote.

Miraji Athuman akipiga mpira

Kwanza, ni heshima kubwa saana kuitwa katika kikosi cha awali cha Amunike, Taifa Stars” alianza kutuambia hili tulipoanza tu kuongea naye.  Hii kwakwe ni furaha na inaonyesha jinsi mchango wake katika soka unavyoonekana mbali.

Miraji hadi sasa ameifungia Lipuli mabao 7 katika ligi kuu.


Wafungaji wa magoli LIPULI FC


Hapo nyuma Kocha kocha mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike, aliwahi sema mchezaji anatakiwa ajisikie fahari pale anapoitwa katika kikosi cha timu ya taifa na aonyeshe mchango wake. Kwa hili tunadhani somo pia lilimuingia sana Miraj. “Nipo tayari kushirikiana na wenzangu pia katika kuonyesha mchango wangu kwa timu ya taifa baada ya kupewa hii nafasi muhimu” Miraj aliiambia Kandanda.co.tz, mara baada ya kuiwezesha klabu yake ya Lipuli kutinga Fainali ya kombe la shirikisho la Azam.

Kocha wa Stars, Emmanuel Amunike

Kikosi cha Stars kilichoitwa kitapitia mchujo ili kupata wachezaji watakao safiri na timu hadi Misri kwaajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Mirsi kabla ya michuano ya AFCON.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.