Mabingwa Ulaya

Nilichokiona mwenye mechi ya Real Madrid Na Manchester United.

Sambaza....

Inawezekana mafanikio ya Zidane yakawa yanakuja bila kelele yoyote kitu ambacho kinaweza kikashtua na kuona kama Zidane siyo kocha mkubwa .

Vikombe sita ndani ya miaka miwili ni mafanikio makubwa sana kwake ingawa mafanikio haya yamekuja bila kelele yoyote.

Kuna uwezekano mkubwa Bale, Benzema na Isco wakacheza katika kiwango kikubwa bila Ronaldo.

Muda wa dakika 83 Real Madrid ilicheza bila Ronaldo na ilicheza vizuri tena kitimu zaidi .

Wakati Zidane anamhamisha Isco kutoka kwenye jukumu la kiungo mshambuliaji wa kati mpaka kuwa kiungo wa pembeni watu wengi walishtuka lakini Isco amedhihirisha kuwa Zidane hakuwa amekosea.

Related image

Kucheza pembeni kwa Isco kuna mfanya kuwa huru zaidi. Mfano katika mechi hii alikuwa huru zaidi akitokea pembeni na kuja eneo la katikati ya uwanja na kuongeza nguvu ya viungo wa kati kitu kilichosaidia kwa namna moja au nyingine viungo wa Manchester United wawe na mzigo mkubwa.

Pia Isco aliweza kucheza nyuma ya Bale na Benzema kitu ambacho kilimwezesha yeye kugawa mipira kwa hawa watu. Inawezekana Isco asiwe na kasi au asiwe mrefu ila akawa na ubunifu mkubwa kwenye miguu yake.

Casemiro, Modric na Kroos jana wote walikuwa huru sana kwenye nafasi zao. Kitu ambacho kiliwafanya wacheze wakiwa wametulia na kufanikisha kuwapoteza viungo wa Manchester United yani kina Matic, Herrera na Pogba.

Matic alikuwa ni mchezaji pekee wa ndani ambaye alionekana yuko ndani ya mchezo kwa kipindi kirefu cha mchezo.

Casemiro jana alionesha yeye ni zaidi ya kiungo wa kuzuia. Kupewa uhuru kwake kumefanya kutuonesha kuwa yeye anauwezo wa kucheza kama Box to box kama akiaminiwa zaidi.

Mijongeo yake ina nafasi kubwa ya kuleta uwiano mzuri kwenye eneo la Kuzuia na kushambulia.

Lingard haikuwa mechi yake, unapokuwa unakutana na timu ambayo mabeki wake wa pembeni wanashambulia sana unatakiwa kuweka mshambuliaji wa pembeni ambaye atasababisha mabeki wa pembeni wakae kumchunga zaidi kuliko wao kukaa kufikiria kushambulia.

Martin Kiyumbi

Sambaza....