
Klabu ya soka ya Yanga baada ya kuanza usajili kwa kasi baada ya dirisha la usajili kufunguliwa August 01 kwa msimu ujao pia inatarajia kutangaza wachezaji watakaochwa kuelekea msimu ujao.
Za chini ya kapeti inasemekana kesho Klabu ya Yanga itatangaza nyota 13 ambao itaachana nao kabla ya kuanza kwa msimu ujao. Huku pia sababu mbalimbali za kuwaacha nyota hao zikiwekwa wazi.
Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na utovu wa nidhamu kwa wachezaji, viwango vibovu vya wachezaji pamoja na wale wanaoonekana waanzilishi wa migomo.
Baadhi ya nyota wataoachwa ni pamoja na Yikpe, Molinga, Raphael Daud, Andrew Vicent, Ally Ally,Adeyum Saleh, Paul Godfrey, Ally Sonso.
Unaweza soma hizi pia..
Alli Kamwe: Lengo Yanga na sio Mayele!
Mayele ni mchezaji muhimu kwenye Timu. Yanga inamuhitaji zaidi akiwa Fiti uwanjani kuliko yeye anavyokihitaji kiatu cha Ufungaji bora kabatini kwake.
Msemaji Simba: Mambo ni magumu!
Kila mwanasimba anatakiwa kufahamu hilo na kukubali mambo ni magumu.
Kola na mfupa uliomshinda Mayele!
Licha ya Fiston Mayele kusifiwa na kuoneoana ni moja ya washambuliaji hatari katika Ligi lakini hakufanikiwa kufunga
Mbinu mpya za Yanga zilizoacha lawama kwa kipa wa Dodoma Jiji
Nasredeen Nabi ilimlazimu kutoka katika mfumo wake wa siku zote wa kumtegemea Fiston Mayele na kubadili mbinu ili kupata ushindi.