Tetesi

Obi Mikel kuibukia Ligi Kuu Misri!

Sambaza....

Kiungo wa zamani wa Chelsea Obi Mikel ameonyesha nia ya yeye  kucheza barani Afrika huku akionyesha uwezekano wa kuelekea katika  katika Ligi Kuu nchini Misri.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria “Super Eagles” ameonyesha lolote linaweza kutokea katika maisha yake ya soka na kutanabaisha bado ana nguvu na hamu ya  kuendelea kucheza soka.

Obi Mikel akiwa na kikosi cha Nigeria “Super Eagles”

Obi Mikel “Kucheza kwenye Ligi Kuu ya Misri? Kwa nini isiwe hivyo?, Mimi ni mchezaji wa mpira wa miguu na kila kitu kinawezekana, sijawahi kukataa chochote.

“Lengo langu ni kuendelea kucheza mpira wa miguu, na natumai nitapata fursa, sijakataa ofa yoyote iliyotolewa kwangu, lakini  mpaka nione ofa yenyewe kama ni nzuri ndipo nitakapofanya uamuzi sahihi.” Imeripotiwa na Kingfut

Kiungo Obi Mikel akiwa Chelsea

Mikel aliondoka Chelsea baada ya kukaa klabuni hapo misimu zaidi ya 10. Ambako alifaninikiwa kushuka dimbani mara 374 na kushinda  mataji nane ya ligi ya nyumbani Uingereza na mataji mawili ya Ulaya.

Baadae alirudi kwenye soka la Uingereza kwa mkataba wa muda mfupi katika klabu ya  Middlesbrough baada ya kutokea nchini China katika klabu ya Tianjin Teda.

Sambaza....