EPL

Rekodi nzito ya Martial kwa wapinzani wao!

Sambaza....

Anthony Martial “Air France” mshambuliaji wa Manchester United amekua sehemu muhimu ya eneo la ushambuliaji la Man United chini ya Ole Guna Solkijer katika msimu huu haswa baada ya majeruhi ya mshambuliaji mwenzake Marcus Rashford.

Katika msimu huu Man Utd na City msimu huu zimekutana mara 4 mpaka sasa, mara mbili katika EPL na mara mbili katika Carabao Cup. Katika michezo yote hiyo ni mmoja tuu ambao City ameibuka na ushindi na United kupata ushindi mara tatu.

Inaonekana Ole ndie mmbabe wa Pep baada ya kumfunga nje ndani katika EPL msimu akifanya hivyo baada ya miaka mingi kupita tangu enzi za Sir Alex Furgason. Katika mchezo wa kwanza City alipoteza kwa mabao mawili kwa moja na mchezo wa pili tena United ilishinda mabao mawili kwa sifuri.

Anthony Martial akishangilia na Bruno Fernandes.

Katika michezo yote miwili hiyo mshambuliaji Mfaransa Anthony Martial amefanikiwa kufunga magoli. Alifunga katika katika mchezo wa kwanza goli la kwanza akipokea pasi ya Daniel James na katika mchezo wa pili alifunga goli la kwanza pia akipokea pasi ya Bruno Fernandes.

Katika ubabe wa Ole kwa Pep ni kwa kiasi kikubwa Martial ndio silaha kubwa ya Ole na kuweza kuufanya mji wa Manchester kua ni mwekundu na sio bluu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.