Ligi Kuu

Rekodi walioiweka Simba baada ya kuifunga Yanga Sc

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba Sc maarufu kama Wekundu wa Msimbazi jana walifanikiwa kuwafunga watani wao Yanga Sc bao moja kwa bila lililofungwa na Erasto Edward  Nyoni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Baada ya ushindi huo Simba imezidi kujisogeza katika kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Pia wakiendelea kua timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa katika VPL.

Kwa ushindi huo unaifanya SimbaSc kuandika rekodi nyingine mpya katika VPL. Mpaka sasa timu hiyo imefanikiwa kuzifunga timu 14 kati ya 15 zinazoshiriki katika Ligi Kuu Bara. Timu pekee ambayo haijafungwa na SimbaSc ni Lipuli ya Iringa.

Lipuli ndio timu pekee iliyofanikiwa kuizuia Simba tena katika mechi zote mbili. Lipuli iliibania SimbaSc kwa kutoka sare ya bao moja kwa moja katika michezo yote miwili iliyochezwa Dar es salaam na Iringa.

Mechi za Simba zilizobaki.

SimbaSc imebakia na michezo minne pekee ili kumaliza ligi msimu huu. Simba imebakiwa na michezo miwili ya nyumbani (Kagera Sugar na Ndanda FC) na miwili ya ugenini ( Singing utd na Majimaji FC).

Katika timu zote nne hizo ambazo hawajamaliza michezo yao ya raundi ya pili na Simba tayari zote zilishafungwa na Mnyama.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x