Mbwana Samatta akiwa Aston Villa
Blog

Samatta achagua upande kati ya Ronaldo na Messi.

Sambaza....

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” na mshambuliaji wa Aston Villa Mbwana Samatta ameweka wazi ni mchezaji gani anaemvutia kati ya Christiano Ronaldo na Lionel Messi.

Mbwana Samatta amemchagua nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo na kumpiga chini Lionel Messi alipoulizwa nani ni mchezaji bora kwake alipokua akiongea na kituo cha Villa tv.

“Messi au Ronaldo? Nitakwenda kwa Cristiano Ronaldo” Mbwana Samatta.

Cristiano Ronaldo

“Nampenda Messi kwani yeye ni mchezaji mzuri na inashangaza kumtazama lakini kwangu nilipoanza kucheza mpira, nilikuwa nikimuangalia Ronaldo kama mfano na wakati unaweza kucheza, kupiga mashuti au kichwa unaweza kuwa mzuri kama Ronaldo”

Nitakua upande wa Ronaldo kwa sababu najua ni mzuri na anafanya nini na kuonyesha kila mchezaji kuwa ikiwa unataka kuwa mzuri unaweza kuwa lakini lazima ufanye bidii.” Aliongeza mchezaji huyo wa zamani wa Simba na TP Mazembe.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.