EPL

Samatta kubaki Ligi Kuu ikiwa hivi…

Sambaza....

Vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), vitakutana Alhamisi hii katika kikao cha dharura kuhusu hatma ya mechi zilizobaki kuhusu msimu huu.

Baadhi ya mipango ambayo inaelekea kujadiliwa ni kumaliza Ligi na kumpa ubingwa Liverpool Fc pamoja na uwezekano wa kuwa na timu 22 katika msimu wa 2020/21. Hii ikiwa na maana vilabu ambavyo vipo mkiani havitashuka ila timu ambazo zilitakiwa kupanda zitapandishwa, hivyo msimu utakao fuata watashusha timu tano.

Ikumbwe mpango huu unaweza kuwa na manufaa kwa Mbwana Samatta ambaye timu yake ya Aston Villa ambayo ipo hatarini kushuka. Samatta alijiunga na Aston Villa akitokea Krc Genk. Hadi sasa ameshaifungia goli moja katika Ligi Kuu hiyo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.