Mbwana Samatta nahodha wa team Samatta katika mchezo wa Samakiba Foundation.
Blog

Nimempiga Samatta kama Mmasai!

Sambaza....

Baba mzazi wa nyota wa Aston Villa na timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Mzee Ally Samatta ameweka wazi malezi aliyokua anamlea mwanae Sammata pamoja na ndugu zake wengine walipokua watoto.

Mzee Ally Sammata anafichua moja ya vitu alivyokua anavisisitiza katika familia na endapo mtoto atakiuka basi alikua anachukua hatua ya kumuadhibu kaka baba, haswa katika swala la elimu na muda wa kurudi nyumbani.

“Nilikua nawachapa kama mmasai maana unajua mtoto ukiwa unamchapa hawezi kutulia tuu lazima mtahangaishana, ndivyo nilikua nawachapa” mzee Ally Sammata anasema ambae alikua ni askari polisi wakatu huo.

Mbwana Samatta

Kwasasa akiwa ni askari polisi mstaafu Mzee Ally Sammata anasema siku ambayo alimchapa Sammata kutokana na kuacha kwenda shule na kwenda kucheza “ndondo” vikindu.

Ally Samatta Pazi “Mwaka huo wakati yupo “form two” alikua anakwenda kucheza ndondo, siku moja Muddy (Mohamed Sammata-KMC) ndio aliyemchongea. Aliniambia Mbwana leo hajakwenda shule amekwenda kwenye ndondo na sio mara yake ya kwanza.

Mbwana Samatta akiwa Aston Villa

Siku moja nikamvizia akaniambia anakwenda ndondo vikindu, nikakuta kwenye begi lake ameweka viatu na nguo na vile viatu nilikua namnunulia mimi, nikamuuliza hivi vyanini akasema walimu wakati mwingine huwa wanatuambia tucheze shuleni. Lakini alijitetea na nikaja kugundua alitoroka shule na kwenda kwenye ndondo baada ya kwenda shule  na kumkosa. Baada ya kurudi nyumbani usiku alijuta”

Mzee Ally Samatta amezungumza hayo alipokua akiongea na katika kipindi cha michezo cha Efm.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.