Ivory Coast's Tiene Siaka (R) vies for the ball with Tanzania's Shomari Kapombe during a World Cup 2014 qualification match between Tanzania and Ivory Coast at the Felix Houphouet Boigny stadium in Abidjan on June 2, 2012. Ivory Coast won 2-0. AFP PHOTO / SIA KAMBOU (Photo credit should read SIA KAMBOU/AFP/GettyImages)
Ligi Kuu

Shomari Kapombe huyoo anarudii!

Sambaza....

Beki wa kutumainiwa wa Klabu ya Simba na Taifa Stars Shomari Kapombe anakaribia kurudi baada ya majeruhi ya muda mrefu tangu mwaka jana.

Beki huyo wa kulia wa kupanda na kushuka aliumia wakata akiwa kambini nchini Afrika ya Kusini akiwa na Taifa Stars na hivyo kupeleka nje ya uwanja kaa muda mrefu.

Lakini leo klabu ya Simba imetoa habari nzuri kwa mashabiki wa Kapombe na Simba pia baada ya kutaja urejeo wake hivi karibuni.
“Shomari Kapombe anatarajia kurejea Afrika Kusini wiki hii kwa ajili ya vipimo vya mwisho kabla ya kuruhusiwa kuanza mazoezi mepesi” Kilieleza chanzo.

Kwa wakati wote huo tangu Kapombe apate majeraha klabu ya Simba imekua ikiwatumia Zana Coulibaly na Nicholaus Gyan kucheza nafasi yake.

Kwa kurudi kwa Shomari Kapombe kunaifanya Simba kubaki na majeruhi mmoja pekee wa muda mrefu ambae ni Salim Mbonde ambae pia nae ameanza mazoezi mepesi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.