Masau Bwire msemaji wa Ruvu Shooting
Ligi Kuu

Simba hawajalipwa mishahara-MASAU BWIRE

Sambaza....

Jana kulikuwepo na mchezo ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba SC na Ruvu Shooting,  mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam nakumalizika kwa sare ya 1-1.

 

Baada ya mchezo huo msemaji wa Ruvu Shooting amedai kuwa klabu hiyo ndiyo klabu pekee hapa nchini ambayo imelipa.mishahara yao ya mwezi huu wa sita.

“Sisi ndiyo timu pekee ambayo mwezi huu wa sita imelipa mishahara yao hapa Tanzania . Wachezaji wetu wamelipwa mishahara yao ya mwezi wa sita kuanzia tarehe 11 ya mwezi huu na leo ni tarehe 14 bado hatujafika hata nusu ya mwezi huu”- alisema Masau Bwire.

Salum Aboubakar “Sure boy” akimtoka mchezaji wa Ruvu Shooting

“Nitafutie timu ambayo kwa sasa imelipa mishahara yao mapema hivi. Hata Simba wenyewe bado wachezaji wake hawajalipwa mishahara yao ya mwezi huu ndiyo maana tumewafunga”- alizidi kusema Masau Bwire.

 

Msemaji huyo mwenye maneno mengi alizidi kudai kuwa Simba iliponea kwenye tundu la sindano kupokea kidogo kutoka kwa Ruvu Shooting.

“Ni huruma ya mwenyezi Mungu tu ndiyo iliyosababisha Simba wasifungwe mechi ya leo.  Ili kutomsumbua kocha mkuu wa timu ya taifa tunashauri awachukue wachezaji wote wa Ruvu Shooting wawe wachezaji wa timu ya taifa”- alimalizia Masau Bwire


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.