Ligi Kuu

Simba kumshusha Mkenya?

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba itawakosa nyota wake wanne waliopo nje ya nchi pindi ambapo Ligi Kuu Bara itarejea tena na kuanza kuchezwa baada ya serikali kuruhusu mpira kuchezwa kuanzai June Mosi.

Simba ina wachezaji wanne waliopo nje ya nchi ambao ni Meddie Kagere(Rwanda), Sharaf Shiboub(Sudan), Francis Kahata(Kenya) na Clatous Chama(Zambia). Lakini kupitia kwa msemaji wa na Mtendaji mkuu wa Simba walitoa ahadi kwa mashabiki wao siku ya Jumamosi yakumleta mchezaji mmoja kati yao walitajwa hapo ili kuungana na wachezaji wengine watakaoingia kambini Jumatano.

Francis Nyambura Kahata.

Mchezaji ambae anatajwa kurudi nchini leo ni Francis Kahata kutoka Kenya ili kuja kukiongezea kikosi cha Simba ambacho kinaongoza kwa alama 71. Francis ama Kachi amehusika katika kufunga magoli manne na pasi sita za mabao katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.

Mtendaji mkuu Senzo Masingisa tayari ameweka wazi wanataka kubeba vikombe vyote viwili msimu huu ili kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi Kimataifa.

Sambaza....