Uhamisho

Simba na Yanga njooni mnisajili -Mwamunyeto

Sambaza....

 

Beki kisiki wa klabu ya Coastal Union Bakari Nyundo Mwamnyeto amedai kuwa kwa sasa yupo na klabu yake ya Coastal Union ambayo mpaka sasa ana mkataba nayo , hivo ni vyema kwa vilabu vinavyomtaka vije kuzungumza na Coastal Union.

” Kwa sasa niko na mkataba na Coastal Union , ni vyema kwa timu yoyote inayonitaka ije kufanya majadiliano kati ya Meneja wangu na klabu yangu ya Coastal Union kwa sababu nina mkataba nayo” alisema mchezaji huyo wakati anazungumza na kituo cha radio cha Wasafi Fm.

 

Alipoulizwa kwa sasa dau lake linaweza kuwa kiasi gani , Bakari Nyundo Mwamnyeto alidai kuwa hawezi kujua kwa sababu hilo ni suala la meneja ambaye anajua kiundani zaidi.

Walinzi wa kati wa Coastal Union Ibrahim Ame na Bakari Mwamunyeto

“Mimi siwezi kukujibu kwa sababu suala la thamani ya dau langu analijua meneja wangu na siyo mimi, cha muhimu ni klabu inayohitaji kufanya mazungumzo naye” alimalizia beki huyo wa kati.

Beki huyu hivi karibuni amejizoelea umaarufu mkubwa kutokana na kutakiwa na vilabu vikubwa viwili hapa nchini vya Simba na Yanga.

Beki huyu ambaye alipewa nafasi kubwa sana na kocha wa sasa wa timu ya taifa Ettiene Ndarigije katika kikosi cha timu ya taifa na kuonesha kiwango kikubwa ambacho kiliwashangaza wadau mbalimbali wa mpira wa miguu nchini.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.