Ligi Kuu

Simba Sc kupewa fedha taslimu pia ya ubingwa

Sambaza....

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuu Boniface Wambura amedai kuwa bingwa wa ligi atapewa zawadi ya pesa.

Akizungumza kuhusu mdhamini wa ligi kuu baada ya mechi ya JKT Tanzania na Kagera Sugar kwenye uwanja wa JK Park amedai kuwa mdhamini alipatikana.

“Mdhamini alipatikana lakini , tukakaa na TFF na vilabu vyenyewe tukaona pesa ni ndogo ambayo ingeshusha thamani ya ligi”.

“Mdhamini aliyepita alikuwa anatoa kiasi cha bilioni 2.5, lakini chini ya hiyo fedha ilikuwa ni kuishusha thamani ya ligi yetu”.

“Ukiitoa ligi ya Afrika Kusini kwa ukanda huu wa Sahara ligi yetu ndiyo bora na yenye ushindani kuliko ligi zingine”.

Kuhusu zawadi ya mshindi wa ligi kuu amedai kuwa wataangalia pesa ya kumpa bingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu.

“Anayetoa pesa kwa bingwa ni mdhamini mkuu, lakini msimu huu hakuna mdhamini mkuu, kwa hiyo tutakaa na TFF kuangalia zawadi gani ambayo bingwa atapewa ukitoa kombe”- alisema Boniface Wambura.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.