
Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SportsSClub ambao leo wanaanza michuano ya Kimataifa wameanza usajili wao wa dirisha dogo kwa kushusha ndugu yake Didier Drogba.
Simba imemsajili Zana Oumar Koulibaly kama mlinzi kulia kutoka katika klabu ya Asec Memosa ili kuziba nafasi ya Shomari Kapombe aliepata majeraha.
Zana Koulibaly mwenye miaka 26 anamudu kucheza kwa ufasaha nafasi ya beki wa kulia anakuja kusaidiana na Shomari Kapombe huku ikimaanisha ndio mwisho wa Nicholas Gyan raia wa Ghana.
Zana Koulibaly ni raia wa Ivory Coast ambae yupo chini ya usimamizi wa Bro Soccer Management ambae pia amepitia katika klabu ya African Sports ya Ivory Coast pia.
Unaweza soma hizi pia..
Msemaji Simba: Mambo ni magumu!
Kila mwanasimba anatakiwa kufahamu hilo na kukubali mambo ni magumu.
Kola na mfupa uliomshinda Mayele!
Licha ya Fiston Mayele kusifiwa na kuoneoana ni moja ya washambuliaji hatari katika Ligi lakini hakufanikiwa kufunga
Alli Kamwe: Kumbe bila moto wanateseka!
: Asante Moalin. Asante Pablo Franco, Mechi ilichezwa sana kwenye mbinu kisha ikamalizikia kwenye Ufundi wa wachezaji.
Azam kujimaliza yenyewe mbele ya Simba!
Miongoni mwa maeneo yatakayopa ushindi Simba katika mchezo huo ni eneo la kiungo na eneo la mlinda mlango.