Kocha wa Simba Sc, Aussems
Ligi Kuu

Simba sc wang’aa tuzo za mwezi March!

Sambaza....

Mwalim wa Wekundu wa Msimbazi Simba sc Mbelgiji Patrick Auseems na nahodha wake pia John Raphael Bocco wamefanikiwa kuing’arisha timu yao kwa kutwaa tuzo za kocha bora na mchezaji bora wa mwezi March katika tuzo zinazotolewa kila mwezi na TFF.

Patrick Auseems ametwaa tuzo ya kocha bora kwa mwezi wa tatu baada ya kuwashinda makocha wenzie Abdul Mingange wa Azam fc na Zubery Katwila wa Mtibwa Sugar alioingia nao fainali.

John Bocco wa Simba ambae pia ni Galacha wa mabao wa mwezi March

Kwa upande wa John Bocco yeye amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo mbele ya wachezaji Donald Ngoma wa Azam fc na Jaffary Kibaya wa Mtibwa Sugar.

Kwa ushindi huo basi John Bocco na Patrick Auseems watazawadiwa fedha taslim shilingi milioni moja.

Katika mwezi March Simba imecheza michezo mitatu na kufanikiwa kushinda michezo yote na kuvuna alama 9 huku John Bocco akifunga mabao manne.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.