Uhamisho

Simba: Tunawaza kumsajili Simon Msuva!

Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmedy Ally amezua gumzo mitandaoni baada ya kusema wao kama Simba wanawaza kusajili wachezaji wa timu kubwa kama Wydad Casablanca.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Ahmedy Ally aliandika kujibu uvumi unaomhusu moja ya wachezaji muhimu wa Simba ambae anatajwa kutaka kusajiliwa na Yanga.

Benard Morrison akishangilia goli lake la kwanza akiwa na jezi ya Simba, pamoja na kiungo Said Ndemla.

“Mmeanza “cheap propaganda” kuhusu wachezaji wetu, sisi tunafurahi kama mnawawaza wachezaji wetu hii ina maana kwamba mnakubali kwamba tuna wachezaji ambao wanaoweza kuwasaidia,” Ahmed Ally

Msemaji huyo wa Simba pia aliongeza wao wanawaza kusajili wachezaji kutoka timu kubea kama Casablanca ambapo miongoni mwa nyota wa klabu hiyo ni Simon Msuva ambae ana matatizo na klabu yake hiyo iliyomsajili msimu huu.

Simon Msuva alipotambulishwa na klabu ya Wydad Casablanca

Ahmedy anaandika “Sisi tunawaza kusajili wachezaji kutoka Wydad Casablanca nyinyi mnawaza kusajili wachezaji kutoka Simba, kila mtu anamuwaza mkubwa wake.”

Kwasasa Simon Msuva yupo nchini akiwa hana klabu anayoichezea baada ya kushindwa kufikia muafaka na waajiri wake Wydad Casablanca ya nchini Morroco aliyojiunga nayo akitokea Difaa El-Jadida ya nchini humo pia.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.