Ligi Kuu

Simba wakanusha habari ya Okwi na Kwasi kuigomea.

Sambaza....

Klabu ya Simba inapenda kukanusha taarifa iliyoandikwa na Gazeti la leo la Bingwa la tarehe 4-1-2018, iliyotoka na kichwa cha habari kikubwa kwenye ukurasa wake kwanza, iliyoandika OKWI, KWASI WAIGOMEA SIMBA.

Taarifa hiyo inaeleza wachezaji hao Emmanuel Okwi na Asante kwasi hawatacheza hadi walipwe fedha zao za usajili.

Kiukweli taarifa hiyo imejikita kwenye kuharibu taswira ya klabu,na yenye nia ovu kwa timu yetu ambayo ipo kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea huko Zanzibar kwa sasa.

Mara kwa mara gazeti hilo limekuwa likiandika taarifa za namna hiyo kwa klabu,hali inayopelekea uongozi wa Simba kulaumiwa na Wanachama wake juu ya mwenendo wa taarifa zinazotolewa na chombo hicho kilichopo chini ya kampuni ya Habari Co-operation.

Binafsi nimekuwa mara kwa mara nikijaribu kuwasiliana na wahariri wa magazeti ya kampuni hiyo ili kujaribu kuweka sawa taarifa zao,lakini kwa sababu wanazozijua wao kumekuwa hakuna mabadiliko yoyote.

Image result for ASANTE KWASI

Kwa taarifa iliyoandikwa leo ambayo imezua taharuki kubwa hususan mitandaoni,klabu imeonelea iliweke sawa kwa kuwaambia Wanachama na washabiki wake kuwa,haidaiwi na mchezaji yoyote pesa yoyote si tu ya usajili hata za mishahara.

Hivyo imelitaka gazeti hilo kuthibitisha taarifa yao ndani ya siku mbili au kukanusha kwa uzito ule ule taarifa yao iliyojaa upotoshwaji usiovumilika.

Vinginevyo klabu ya Simba itachukua hatua stahiki kwa gazeti,mwandishi,mhariri na kampuni hiyo ambayo tunaiheshimu sana.

Tupende pia kuwaarifu pia mchezaji Emmanuel Okwi ataonekana uwanjani hivi karibuni baada ya ruhusa yake ya matibabu kumalizika,
huku Kwasi akiendelea kuitumikia klabu kama mlivyoona leo kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri toka kisiwani Pemba.

Kukosekana kwa Kwasi juzi kwenye mchezo dhidi ya Mwenge kulitokana na maamuzi ya benchi la ufundi na kuandikwa jina lake kwenye kikosi, kulitokana na makosa ya kiuandishi kama ambavyo wao gazeti la Bingwa linavyokosea(errors ).

Matarajio yetu ni kuona jambo hili halitajirudia tena na tuna mategemeo makubwa kuona masasahihisho haya yanafanyika kwa wakati kama tulivyoandika huko juu.

-Taarifa kutoka klabu ya Simba SC, kupitia msemaji wake. 4/1/2017

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x