Stori

Simba Yachota Mamilioni Mengine ya Jezi

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba leo imetambulisha mdhamini mpya wao Sandaland jezi “kit sponsor” baada ya kuachana na aliyekua mdhamini wao kwa miaka miwili Vunjabei.

Simba na Sandaland wameingika mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya bilion nne na mtendaji mkuu akiwatambulisha mbele ya waandishishi wa habari alisema “Mwanzoni tulikuwa tunapata milioni 400 kwa mwaka kutokana na jezi. Akaja Vunja Bei akatupa bilioni moja kwa mwaka na huyu wa sasa anakuja kutupa bilioni mbili kwa mwaka. Namshukuru sana Sandaland kuwa mdhamini wa jezi kwa msimu wa 2023.” CEO Imani Kajula aliongezea na kufafanua zaidi

“Hatuwezi kuwa timu kubwa Afrika bila kuwa na uwezo wa kifedha, leo hii tunasimamia sana kwenye eneo hilo. Kwetu hatua ni safari na leo tunapiga hatua kubwa zaidi.”

Salim Abdallah

Nae Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Salim Abdallah “Try again” alimpongeza Sandaland n kumshukuru pia Vunjabei “Nampongeza Sandaland kwa kupata nafasi hii, alijaribu mara ya kwanza hakufanikiwa lakini muda huu amepata. Namshukuru pia VunjaBei kwa udhamini aliotupatia,” alisema Mwenyekiti wa Bodi, Salim Muhene ‘Try Again’.

Ahmed Ally pia alisema matunda yote haya hayakuja bure tuu bali ni uwekezaji wa Rais wa heshima Mohamed Dewji, lakini pia wao Simba ndio waanzilishi wa kila jambo.

Imani Kajula, Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba

“Sisi tunakuwa wa kwanza kwenye matukio makubwa na matukio muhimu na leo inakwenda kuwa hivyo.”

“Namshukuru Rais wa heshima wa Simba, Mohamed Dewji kwa kuikuza brand ya Simba. Sasa hivi kila kampuni inatamani kufanya kazi na Simba kwa sababu ya alivyoipigania. Tunajua bado anamalengo makubwa ya kuhakikisha Simba inatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika,” Ahmed Ally alimalizia.

 

Sambaza....