Sambaza....

Kikosi cha Simba kimeondoka jijini Dar es salaam leo asubui na kuelekea Congo kwa kupitia Nairobi kuifuata AS Vita huku ikiwaacha baadhi ya wachezaji wake muhimu nchini kutokana na sababu mbalimali.

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuwasili jijini Kinshasah saa saba mchana kwa saa za Congo wakiwa tayari kabisa kwa mchezo wao wa ligi ya mabingwa katika kundi D.

Simba imeondoka bila ya mshambuliaji na nahodha wake John Bocco aliye majeruhi. John Bocco aliumia katika mchezo wa kwanza dhidi ya JS Souara na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Meddie Kagere.

Pascal Wawa.

Kikosi cha Simba kilichoondoka leo ni Makipa: Aishi Manula, Deo Munishi. Walinzi: Nicholaus Gyan, Mohamed Hussein, Pascal Wawa, Juuko Mursheed, Paul Bukaba. Viungo: James Kotei, Jonas Mkude, Mdhamiru Yasin, Mohamed Ibrahim, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya, Rashid Juma, Cleotus Chama. Washambuliaji: Emmanuel Okwi, Adam Salamba na Meddie Kagere.

Simba inakwenda Kinshasah kwenda kucheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi huku wao waliwa ndio vinara wa Kundi D baada ya kuwanyuka mabao matatu kwa sifuri Waarabu wa Js Souara kutoka Algeria.

Sambaza....