Tetesi

Simba yampora mchezaji wa Yanga uwanja wa Taifa

Sambaza....

Moja ya tukio ambalo analikumbuka vizuri mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismael Aden Rage ni kitendo cha Yanga kumpora Mbuyu Twite katika uwanja wa Taifa.

Mbuyu Twite alikuwa njiani kuelekea kwenye timu ya Simba lakini alipofika uwanja wa ndege , Yanga walimchukua na Simba wakabaki midomo wazi.

Bakari Nondo Mwamunyeto anatakiwa na klabu za Simba na Yanga.

Tukio hili limejirudia tena baada ya Simba kuwapora Yanga beki mahiri wa Coastal Union , Ibrahim Ame. Ibrahim Ame alikuja Dar kwa ajili ya kusajiliwa na Yanga.

Alipofika uwanja wa ndege Simba walimnyakua na sasa yuko kwenye mikono ya Simba. Beki huyo msimu uliopita alicheza na Bakari Mwamunyeto ambaye ameshasajiliwa na Yanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.