Uhamisho

Simba yawapora mchezaji Yanga !

Sambaza....

Simba inaendelea na usajili kwa ajili ya kujiimalisha na msimu ujao ambapo itashiriki ligi ya mabingwa barani Afrika pamoja na ligi kuu Tanzania bara. Mpaka jana klabu ya Simba ilikuwa imefikia hatua nzuri ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa KMC FC Charles Martin Ilanfia.

Awali Charles Martin Ilanfia alikuwa akitakiwa na Yanga , lakini Simba wameshaingia kati na tayari wameshafanya mazungumzo na uongozi wa KMC FC kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo ambaye amemaliza ligi akiwa na magoli 4. Akizungumza na www.kandanda.co.tz mtendaji mkuu wa KMC , Walter Harrison amedai kuwa mpaka sasa hivi wameshafanya mazungumzo na klabu ya Simba.

“Mpaka sasa hivi kulikuwa na makubaliano kati ya klabu na klabu ambayo yalikuwa haijakamilika. Natumaini mpaka kufika kesho tutakuwa tumekubaliana na Simba ni kiasi gani ambacho wanatakiwa kutupa”. Alisema mtendaji huyo wa KMC.

Kuhusu suala la Simba kukubaliana na Charles Martin Ilanfia , Walter Harrison amedai kuwa KMC iliwapa nafasi Simba ya kuzungumza na mchezaji huyo kwa ajili ya makubaliano ya awali.

“Kuhusu mchezaji na Simba tumewapa ruhusa wao kuzungumza na mchezaji. Kuhusu kukamilika kwa mazungumzo kati ya mchezaji na Simba mazungumzo hayakamilika kwa sababu sisi hatujamalizana na Simba” – alisema Walter Harrison.

Kuhusu ni lini mazungumzo haya yatakamilika , Walter Harrison amedai kuwa baada ya siku mbili Charles Martin Ilanfia atakuwa mchezaji wa Simba.

“Tunamalizia makubaliano machache tu kwenye mkataba wetu na Simba , na muda huu nimetoka kuzungumza na CEO wa Simba hivo baada ya siku mbili tutakuwa tumemalizana na Charles Martin Ilanfia atakuwa mchezaji wa Simba rasmi”- alimalizia Walter Harrison


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.