Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba imefanya Maangamizi ya kufa mtu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa timu ya Allience fc ijayomiliwa na shule ya kufundishia soka ya jijini Mwanza.

Katika mwendelezo wa Ligi Kuu Bara huku Allience wakifikisha mchezo wa 11 lakini wao SimbaSc wakifikisha raundi ya 9, Allience fc wameshindwa kuhimili ngurumo za Simba na kukubalii kipigo cha mabao matano kwa moja.

Simba walianza kwa kasi mchezo huo huku mastar wake wa kikosi cha kwanza kibao wakiwa nje ya uwanja ilifanikiwa kuandika bao mapema katika dakika ya 10 kupitia kwa Emmanuel Okwi na Asante Kwasi dakika ya 30 katika kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Simba walifanikiwa kuongeza mabao kupitia kwa Emmanuel Okwi kwa mara nyingine na  Adam Salamba katika dakika ya

Cletus Cholla Chama alikamilisha kalamu ya mabao baada ya kufunga bao la 5 saafi kabisa baada ya kuwapiga chenga mabeki na kuachia shuti kali.  Lakini mchezo ukielekea kuisha Allience walipata bao lá kufutia machozi katika dakika ya 93 ya mchezo.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Allience kua klabu iliyofungwa mabao mengi katika mchezo mmoja (mabao 5) katika msimu huu.

Kwa ushindi huo unaifanya Simba kufikisha alama 20 na kushika nafasi ya Pili nyuma ya AzamFc iliyopo kileleni.

Sambaza....