Sambaza....

Mapinduzi ya kizazi kipya cha watu kujivunia na kuzipenda timu zao za mikoani yalianzia kwa Mbeya City.

Timu ambayo wana Mbeya walijivunia kuishabikia, kuipenda na kuisaidia kwa hali yoyote kadri ambavyo uwezo wao ulivyo waruhusu.

Mbeya City hawakuwaangusha mashabiki wao mwanzoni, waliwapa furaha ambayo walitazamia kuipata kipindi ambacho wanaishabikia timu.

Msimu wao wa kwanza kwenye ligi kuu walionesha ushindani wa hali ya juu, wakafanikiwa kuingia katikati ya wazee wawili wa mpira hala Tanzania ( Simba na Yanga)

Tano bora ya Ligi Kuu

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC2041404618401122279466
2Yanga SC1961334320326117209442
3Azam FC1981105038301148153380
4Kagera Sugar FC198596871168204-36245
5Tanzania Prisons196577267171190-19243

Kabla ya ligi kumalizika watu wengi waliipa nafasi Mbeya City kuchukua kombe, na hii ni kwa sababu ya matamanio ya watu wengi.

Matamanio ambayo yalikuja kutokana na wao kuchoka kushuhudia kila siku Simba na Yanga wakibadilishana kombe la ligi kuu.

Matamanio ambayo yaliifanya Mbeya City kupata mashabiki ambao hata siyo wazaliwa wa Mbeya, mtu wa Mwanza akawa anajivunia kuishabikia Mbeya City kwa sababu tu ya matokeo waliyokuwa wanayapata ndani ya uwanja.Mbeya City ikawa na mvuto mkubwa ndani na nje ya uwanja

Enzi za Mbeya City FC

Hamasa hii iliwapa nguvu Mbeya City na ilifanikiwa kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu ( 3) , haya yalikuwa mafanikio makubwa sana kwao kwa sababu ndiyo kwanza ulikuwa msimu wao wa kwanza.

Mafanikio ambayo yaliwafungua watu wengi kutoka mikoa mingi hapa nchini na kuona kumbe kuna uwezekano wa kupata furaha kwa kutumia timu za ndani.

Hamasa ya wana Mbeya kwa Mbeya City iliwavutia wengi, na viongozi wa Mbeya City wakaitumia nafasi ile kwa ajili ya kupata wadhamini kwenye timu.

Ndiyo ikawa timu ya kwanza kuwa na wadhamini wengi kwenye timu kati ya timu zilizokuwa zinashiriki ligi kuu, kitu ambacho kilionesha timu yao inaendeshwa katika misingi ya kisasa.

Pamoja na ugeni wao, uchanga wao walifanikiwa kufanya jambo ambalo Simba na Yanga liliwashinda.

Sifa zikazidi kwao, kiasi kwamba zikawa kama upepo ambao ulikuja kuwayumbisha wao na kupotea kwenye njia ambayo walikuwa wamepanga kupitia.

Mbeya City rasmi ikaanza kupoteza mvuto, matokeo yao uwanjani yakawa hayavutii, lile tumaini la wengi kupata timu ambayo inaendeshwa kisasa likawa limepotea tena.

Mbeya City ikaingia rasmi kwenye siasa za Simba na Yanga, waungwana wakaanza kujitoa taratibu na kukaa pembeni kusubiri mtu mwingine atakayeweza kuleta timu ambayo inaendeshwa kisasa.

Miaka kadhaa imepita, Tanzania tumefanikiwa kupata timu nyingine ambayo inaonekana inaendeshwa kisasa.

Timu ambayo haimilikiwi na wanachama ila ni ya mtu binafsi.

Timu ambayo msimu huu ndiyo msimu wake wa kwanza kwenye ligi kuu lakini mpaka sasa ina wadhamini saba( 7).

Singida United wamefanikiwa kupata wadhamini wengi bila kuwa na hamasa kubwa ya mashabiki nyuma yao kama ilivyokuwa kwa Mbeya City.

Viongozi wake wamekaa chini, wakatengeneza namna sahihi ya wao kupata wadhamini ambao watakuja kuwekeza katika timu yao.

Walijua mapema kuwa hakuna mfanyabiashara ambaye asingependa kutangaza bidhaa yake sehemu ambayo inafuatiliwa kwa ukubwa kama ligi kuu.

Walitengeneza namna sahihi ya kuwashawishi wafanyabiashara hawa na kuwaonesha namna watakavyonufaika kama watawekeza kwenye klabu.

Ushawishi mzuri husaidia kupata nyama iliyonona, tunavyoongea kwa sasa Singida United hawana matatizo kama vilabu vingine ambavyo vilipanda ƙligi kuu msimu huu.

Gharama za uendeshaji wa timu kwao zimepungua kwa kiasi kikubwa.

Ni kitu kikubwa na cha kuwapongeza, lakini tunapowapongeza tusisahau kuwakumbusha kuwa hicho walichokifanya ni kitu kidogo ndani ya vitu vikubwa wanavyotakiwa kufanya.

Wana hatua mia za kufikia mafanikio makubwa lakini mpaka sasa wamepiga hatua moja peke yake.

Nina tamani hatua yao ya pili kuiona, hatua ambayo itakuja na mikakati ya kuendeleza misingi sahihi ya mpira.

Leo hii wanatumia gharama kubwa kununua wachezaji wakubwa, siyo kitu kibaya kwa mwanzoni. Wanatakiwa kufikiria namna sahihi ya kutengeneza njia ambayo itawawezesha kutengeneza na kulea vipaji vipya ambavyo vitakuja kuisaidia timu yao kwa baadaye.

Maendeleo ya mchezo wowote msingi wake huanzia kwa vijana wadogo, bila kuwekeza kwenye vituo vya kuibua, kulea na kuendeleza vipaji hutokuwa na msingi imara wa maendeleo ya mchezo wowote kwa Taifa.

Kama Singida United wamefanikiwa kupata wadhamini zaidi ya watano ndani ya msimu mmoja, naamini wana nafasi kubwa ya kutengeneza miundombinu imara itakayowawezesha wao kujiendesha kisasa zaidi.

Tuna makampuni mengi ambayo Singida United wanaweza kuyatumia kupata hostel ya timu ya vijana na uwanja kikubwa ni wao kuandaa njia ya kibiashara ambayo itamshawishi mtu.

Mfano, mfanyabiashara yoyote hutegemea bidhaa yake kutangazwa mara kwa mara ili iweze kuwa akilini mwa mnunuzi kwa muda mrefu.

Mfanyabiashara yupi atakataa kipindi utakapomfuata akutengenezee kiwanja ambacho jina la kiwanja litakuwa jina la bidhaa yake?

Bidhaa yake unaipa nafasi ya kutamkwa kwa muda mrefu kwa kutumia jina la hostel au uwanja ambao Singida United wataumiliki wao.

Hapa ndipo Mbeya City hawakupafikia, pamoja na kwamba walikuwa na hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki lakini hatua hii hawakufanikiwa kuifikia, natamani Singida United kuwaona wakiifikia baada ya wao kuipita ile hatua ya Mbeya City kufanikiwa kupata wadhamini

Sambaza....