Sambaza....

Klabu ya soka ya Singida utd ya mkoani Singida imeendelea na harakati zake za usajili na kufanikiwa kuwanasa Wazambia wawili.

Singida utd imewaongeza Wazambia wawili katika nafasi ya kiungo na ya ushambuliaji ili kujiimarisha katika Ligi Kuu Bara na michuano ya Sportpesa Supercup.

Singida utd imemsajili Jonathan Daka anacheza nafasi ya kiungo na pia mchezaji wa timu ya Taifa ya Zambia chini ya umri wa miaka 23. Pia wamemsajili Gift Mwake mwenye miaka 20 anacheza nafasi ya ushambilliaji kutoka katika klabu ya Monze Swallows FC.

Wachezaji wote wawili raia wa Zambia wamesaini kandarasi ya miaka mitatu kila mmoja!

Sambaza....