Ligi KuuUhamisho

Singida Utd yaweka hadharani usajili wake!

Sambaza....

Klabu ya Singida utd leo imezungumza na waandishi wa habari na kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu klabu kuelekea fainali ya Azamsports FederationCup itayopigwa June 2 Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Moja ya habari kubwa ni kuweka wazi usajili wao msimu ujao huku ikiwapiga bao Yanga kwa mnyakua winga wa Ndanda aliekua anawaniwa na Wanajangwani!

Usajili uliotangazwa leo na klabu  ya Singida utd :

Tiber John kutoka Ndanda fc!

Uongozi wa Singida United umemtangaza mchezaji huyu kuwa mchezaji wake kwa kusaini naye mkataba wa miaka mitatu.
Tiber amejiunga na Singida akitokea Ndanda FC ya Mtwara iliyojikwamua kuepuka kushuka daraja katika mechi ya mwisho msimu uliomalizika.

Mchezaji huyo pia alikua akiwindwa na Yanga.

Tiber John akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari na Festo Sanga

Amara Diaby ametoka Asec Memosa!

Singida Utd pia imemtangaza kumsajili Amara você Diaby  raia wa Ivory Coast ambaye anatokea Asec Mimosa. Mchezaji huyo pia alikua akishiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Africa akiwa na klabu yake hiyo ya Ivory Coast.
Felipe Oliveira Dos Santos akitokea Brazil!
Klabu ya Singida United pia imemtangaza mshambuliaji mpya Felipe Olveira do Santos raia wa Brazil, ambae anapewa michuano ya Sportpesa Supercup ili kuweza kuthibitisha uwezo wake ndipo atasajiliwa.
“Mkataba Wa Do Santos tayari upo wa miaka miwili lakini anatakiwa athibitishe uwezo wake kule Nairobi Kenya ndio tutamsajili”  Festo Sanga amesema.
Mbrazil huyo pia amewahi  kukipiga katika klabu ya Asec Mimosa ya nchini Ivory Coast.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x