Ligi Kuu

Stand United yajichimbia Gamboshi kuwawinda Simba.

Sambaza....

Klabu ya Stand United ya mjini Shinyanga imeweka kambi katika mji wa Bariadi mkoani Simiyu kwa ajili ya mechi ya Simba.

Hii ni mara ya pili kwa Stand United kuweka kambi katika mji huu. Kabla ya mechi ya Yanga ya msimu huu iliyochezwa Shinyanga, Stand waliweka kambi katika mji huu.

Watu wengi wa mji wa Bariadi mkoani Simiyu, wamekuwa wakiwaona Stand United wakitokea kwenye njia ambayo Gamboshi ipo.

Inasemekana kuwa Stand United wamekuwa na imani kubwa ya kwenda Gamboshi baada ya kufanikiwa kuwafunga Yanga katika mechi iliyopita.

Mashuhuda wengi wamekuwa wakiwaona Stand United wakitokea huko, na jioni wanafanya mazoezi katika uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.