Wachezaji wa Taifa Stars
AFCON

Taifa Stars Yatakata kwa Mkapa

Sambaza....

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja bila dhidi ya wageni wao Niger katika mchezo wa kufuzu michuano ya Afcon ya nchini Ivory Coast.

Stars imepata ushindi kwa bao pekee la Simon Msuva lililofungwa katika dakika ya 68, Simon Msuva  alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Novatus Dismas upande wa kushoto mwa uwanja.

Kwa ushindi huo Stars inafikisha alama saba na kusogea mpaka nafasi ya pili nyuma ya Algeria vinara wa kundi na kuwaacha nyuma Uganda ambao wapo uwanjani kwasasa.

Simom Msuva akimtambuka mlinzi wa Niger.

Stars sasa inaombea Algeria iifinge Uganda na kuendelea kuwa kinara na Stars wawafunge Algeria katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo.

Mchezo wa mwisho wa kufuzu Afcon utapigwa baadae September na hivyo kuamua hatma ya Watanzania kushiriki Afcon kwa mara ya tatu nchini Ivory Coast.

 


Sambaza....