Mataifa Afrika

Tanzania kufuzu Afcon ni kama filamu kwetu!

Sambaza....

Makundi CAF kama filamu ya “One down two to go”. Hatimaye draw ya kupanga makundi kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2023 nchini Ivory Coast imefanyika.

Tanzania tumepangwa Kwenye kundi F, tukiwa na mataifa ya Algeria ,Uganda na Niger tukiwania moja ya nafasi mbili adimu za kufuzu.

Katika kundi hili kuna jirani yetu kijiografia Uganda ambaye tunajenga naye Afrika Mashariki kongwe ile ya nchi 3 za Kenya Uganda na Tanzania kabla ya mapenzi yetu na uungwana wetu ikiwemo ukarimu wa kuyakaribisha mataifa mengine kama Burundi, Rwanda, South Sudan na sasa Congo DR.

Mashabiki wa Uganda wakipiga picha na shabiki wa Tanzania katika Uwanja wa Mkapa.

Sisi tumepangwa kundi moja na Uganda lakini tunaye Kigogo moja ndani ya kundi ambaye nampa 100% ya kufuzu kwenye kundi kutokana na kuwa na wachezaji wengi hodari wanaocheza ligi mbalimbali duniani wakiongozwa na Riyad Mahrez wa Manchester City pia uzoefu wao kushiriki michuano mikubwa ya kombe la dunia mara kwa mara licha ya safari hii kukosa.

Achili mbali matokeo ambayo huwa tunayapata mara tukutanapo nakumbuka zile 7 za mwaka ule 2015? ambapo nyumbani tulilazimisha sare ya 2-2 kwenda kule tukaangukiwa na kontena la futi 40?

Riyadh Mahrez.

Niacheni nionekane muoga tu lakini akili yangu inampitisha moja kwa moja Algeria kuchukua nafasi moja wapo kati ya hizo mbili.

Tukiugeukia ukweli Uganda katuzidi kwenye kuanzi FIFA Ranking kushiriki mara nyingi zaidi ndani ya michuano hiyo na ushindani anapokuwa kwenye mashindano hayo vipaji vya vijana wao ukuzaji vipaji na muendelezo wake, kutawanyika kwa wachezaji wake kona mbalimbali za dunia kunaongeza kitu katika timu yao ya Taifa kwa kwa tafiti yangu isiyo rasmi ligi ya Tanzania tu ina Waganda wasiopungua 10 wakiongozwa na hawa wawili wa Simba na Yanga, Khalid Aucho na Thadeo Lwanga.

Khalid Aucho.

Maana yake nini, hapa ni wigo mpana wa uteuzi kwa timu ya Taifa na uzoefu watakoupeleka kwao kutokana na kucheza nje ya nchi yao tena wengi wao ni kwa muda mrefu.                                                             

Tanzania sisi kiasi fulani tumeonesha dira kwa sasa tumeita vijana wengi wanaocheza nje katika mashindano tuliyoyaanda mwezi moja uliopita tulikuwa na mwanga, japo shaka langu ni muda tu, kwa kuwa sisi ndiyo kwanza tupo kwenye ujenzi wa timu ya wakati ujao kwa filosofi ya Kocha Kim Poulsen.

Mbwana Sammata na Simon Msuva.

Mechi za kufuzu zinahitaji sana mapambano, uzoefu, kizazi (generation) yenye kuwiana kwenye vipaji na “performance”. Mfano kwetu tunamuangalia Mbwana Samatta kama mchezaji muhimu anayemfwatia ni Simon Msuva, hapa nadhani kwenye uwanda wa kipaji  kuna utofauti mkubwa sana kama utaruhusu kuugeukia ukweli na kuukubali ukweli.

Niger ndiyo mwepesi kwenye kundi hili wao ni moja ya mataifa ya Magharibi yasiyifanikiwa sana kisoka na mfano ni vilabu vyao na majuzi tu tumetoka kuona Us Gendamarie iliyokuwa kundi moja na Simba katika kombe la shirikisho na hata nahodha wao wa timu ya Taifa ni yule beki ya kushoto jezi namba 29 Abdoulkarim Mamoudou.
Kifupi litakuwa ajabu la 8 la dunia kwangu miye kuona Niger anatoboa kundi hili

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Niger Victorien Adebayor (kushoto) akiwania mpira dhidi ya mpinzani. 

Nihitimishe kwa kusema kufuzu tunaweza lakini inahitaji machozi, jasho na damu kwa umoja na ushirikiano wa hali ya juu tunaweza (don’t fear anyone) kwa sauti ya Ammy Ninje.

Kwa mtizamo wangu wa kiaverage
1.Algeria 51%
2 Uganda 20%
3 Tanzania 20%
4 Niger 9%

Hapa ndipo unapopata dhana ya filamu ya zamani ya sana za mapigano Jimmy Carey Jimmy Brown na mwenzao moja One down two to go’ je ni sisi au Uganda atakayeenda na Algeria?


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.