Uhamisho

Tigana Lukinja: Sikutegemea usajili wa Yanga!

Sambaza....

Mchambuzi wa soka na mchezaji wa zamani wa Nazareth ya Njombe Tigana Lukinja amesema hakutegema kuona usajili wa nyota waliosajiliwa Yanga haswa wa eneo la ulinzi.

Tigana anasema hakutegema kama mlinzi Abdallah Shaibu Ninja atarudi nyuma na kujiunga na Yanga sc na kutoka Ulaya alipokua akicheza soka la kulipwa.

“Sikutegemea kama Ninja atarudu nchini na kujiunga na Yanga ni kama amerudi hatua 60 nyuma kutokana na alipokua. Tayari alikua katika nchi ambazo walau zimechangamka kisoka lakini ameamua kurudi nyuma” Tigana Lukinja.

Abdalah Shaibu “Ninja”

Abdallah Shaibu alikua nchini Czech Republic katika klabu ya MFK Vyskov ambayo ilimtoa kwa mkopo katika klabu ya LA Galaxy msimu uliopita.  Lakini kabla ya msimu kumalika Ninja alionekana katika mazoezi ya Yanga huku ikisemekana mwalimu wa Yanga (Luc kwa wakati ule) alitaka amuone kabla ya kumsajili.

Baada ya Yanga kumtambulisha Ninja leo hii Tigana anasema Abdalah Shaib ni miongoni mwa aina ya walinzi wanaohitajika sana nchini Ulaya.

Abdalah Shaibu Ninja

Tigana Lukinja ” Ninja kwa mara ya kwanza nilimuona katika michuano ya Sportpesa na sikusita kusema ni miongoni mwa walinzi bora wanaofaa kucheza Ulaya haswa kutokana na aina yake ya mpira na umbo lake. Anafanya tackeling nzuri na pia ni mpambani mzuri.

Lakini ameamua kurudi nchini na kujiunga tena na Yanga, kwangu mimi sijafurahishwa kabisa na usajili huu.”

Abdalah Shaibu anakwenda kuungana na Bakari Nondo Mwamunyeto na Yassin Mustapha kwenda kuunda ukuta mpya wa klabu ya Yanga

 

Sambaza....