Kikosi cha Stars kikiwa mazoezini kujiandaa na michezo ya kufuzu Afcon
Mataifa Afrika

Timu yangu, chaguo langu! Kila lakheri Taifa Stars

Sambaza....


Safari ya kufuzu kwa michuano ya mikubwa zaidi kwa Africa kwa upande wa timu za Taifa
‘AFCON’ inaanza leo kwa timu yetu ya Taifa kushuka dimbani.

Huu ni mchezo wetu wa kwanza katika mbio hizi za kufuzu na hili ni kundi F lenye timu za Algeria ,Uganda na Tanzania na Niger.

Binafsi naamini Algeria atafuzu kwenye kundi hili bila kujalisha kuwa kinara wa kundi au la, na hapa naomba nieleweke sina uoga wowote wa kuwaogopa bali nimezama kiufundi kwenye ‘quality’ yao kwa mchezaji mmoja mmoja na “experience” na “exposure” yao kiujumla kwenye levo la ya timu ya taifa.

David Mwantika akipiga pasi mbele ya kiungo wa Algeria.

Ni washiriki wa mara kwa mara kwa kombe la dunia kitu ambacho kinaleta utofauti wa kwanza na washiriki wengine kwenye kundi hili. Hivyo basi kwangu nawapa 51%kufuzu huku Uganda nikiwapa 20% the same nasi 20% na zinazobaki 9% nazielekezea kwa Niger.

Kwa maana nyingine game yetu ya leo ni muhimu sana kupata matokeo ya alama tatu kama si moja ili kuanza safari hii vyema kwa timu ambayo ni ya kawaida.

Nilibahatika kuwepo kwenye mazoezi ya mwisho ya timu na niliona maandalizi ya kiufundi na mbinu kutoka benchi la ufundi hakika nina matumaini makubwa sana ya kufanya vyema katika mechi hii.

Tigana Lukinja (kulia) akiwa na Mbwana Samatta (kushoto) baada ya mazoezi ya Timu ya Taifa kumalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Baadaye nilipata ya wasaa wa kuzungumza na wachezaji na makocha wa timu yetu hakika nilienjoy mtizamo wao na maandalizi ya kisaikolojia walionayo.

Nilifurahi sana kuona umoja na ushirikiano wa wachezaji wakubwa (wazoefu) katika timu na wale chipukizi ambao hawajaitwa zaidi ya mara tano kikosi hapo. Hapa ilinipa mwanga kuwa maeneo mengi yanaoweza kutoa matokeo kwenye soka yameandaliwa.

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Niger Victorien Adebayor.

Mwisho nikakumbuka nyota mkubwa wa Niger na ndiyo mfungaji bora wa muda wote wa Taifa hilo Victorien Adebayor mwenye goli 17 katika michezo 44 akianza kuitumikia timu hiyo mwaka 2015 anaimbwa sana na mashabiki wa timu ya Simba.

Mimi naamini kwa timu yetu nzima naamini kwa uzoefu wa nahodha wetu Mbwana Samatta na wenzake wengi wanaocheza ndani na nje ya nchi kwenye kupata matokeo leo hii.

All the Best Taifa Stars. My Team My Choice

Sambaza....