Papy Kabamba Tshishimbi.
Tetesi

Tshishimbi amfuata Morrison SIMBA

Sambaza....

Baada ya mshambuliaji wa Yanga , Bernard Morrison kwenda katika klabu ya Simba , aliyewahi kuwa kiungo wa klabu hiyo Papy Kabamba Tshishimbi yuko njiani kuelekea Simba.

Papy Kabamba Tshishimbi ambaye amemaliza mkataba wake na Yanga. Mazungumzo ya mkataba mpya kati yake na Yanga kuhusu mkataba mpya yalishindikana hivo wakaachana kwa amani na Yanga.

Nahodha huyo wa zamani wa Yanga amekuwa na mazungumzo na Simba , mazungumzo ambayo kwa kiasi kikubwa yamefikia katika hatua nzuri sana.

Habari za ndani zinadai kuwa Papy Kabamba Tshishimbi atatambulishwa rasmi kama mchezaji wa Simba siku ya jumatatu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.