La Liga

Uhispania wafanya mabadiliko madogo kwenye michuano yao.

Sambaza....

Shirikisho la kandanda nchini Uhispania (RFEF) jana Jumatatu limefanya mabadiliko madogo ya kombe la Mfalme (Copa del Rey) na lile la Hisani (Spanish Super Cup) ambalo huwakutanisha mabingwa wa Laliga na Copa del Rey kuanzia msimu wa mwaka 2019-2020.

Kombe la Copa del Rey sasa litachezwa kwa mfumo wa mchezo mmoja pekee tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa ni mechi za nyumbani na ugenini isipokuwa kwa mechi za nusu fainali ambapo imebaki kama ilivyokuwa hapo awali, na fainali zake zitakuwa April 18, 2020.

Wakati ambapo Spanish Super Cup itabadilika kutoka kuwa washindi wa ligi kuu na kombe la mfalme kuwa taji ambalo litawania na timu nne, ambazo ni wacheza fainali wa Copa del Rey na walioshika nafasi mbili za juu kwenye ligi kuu kwa msimu huo.

Ikiwa kama timu mbili za juu kwenye msimamo wa ligi ndizo hizo hizo ambazo ambazo zitakuwa zimechuana kwenye fainali ya kombe la mfalme basi nafasi za chini zinazofuata kwenye msimamo wa ligi ndizo zitakazoingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Vilevile Super Cup itafanyika mwezi Januari badala ya mwanzoni mwa ligi, na kwa msimu ujao itafanyika tarehe 8 na 9 kama fainali na Januari 12 itakuwa nido fainali yenyewe.

Tayari vyombo vya habari nchini Uhispania vimenukuliwa vikisema kuwa RFEF imeshaingia mkataba na Saud Arabia kwa mechi hizo ndani ya miaka 10 ijayo, jambo ambalo limepingwa vikali na rais wa RFEF Luis Rubiales “Bado hilo tunaliangalia, hakuna makubaliano yoyote hadi sasa, licha ya Saudi Arabia kuwa miongoni mwa nchi zilizopendekezwa, hilo hatukatai”.

Fainali ya Super Cup kwa msimu uliopita ilifanyika nchini Morocco ambapo Barcelona walitwaa taji hilo mbele ya Sevilla ambao kama utakumbuka vizuri ndio ambao watakuja nchini mwezi Ujao kucheza na ama Yanga au Simba kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.