Shirikisho Afrika

Ukweli ni kwamba Simba uwezo wao ni robo fainali!

Sambaza....

Siku zote ukweli huwa haupati nafasi moyoni kwa mwenye mapenzi, hata leo ukienda kumueleza mtu madhaifu ya mwanamke/mwanaume wake juu ya mabaya yake na bahati mbaya akawa amependa kwa dhati ataona unataka kumpeperusha mtu anaempenda tu, ukweli ni dawa japo kuwa huuma.

Ukweli ni kwamba Simba ni kubwa kwa nchini kwetu hata na Afrika Mashariki na Kati, hilo halina ubishi na lipo wazi kabisa, sasa ukweli huu kuna watu bado hawakubaliani nao ndo maana kutwa kucha yanaibuka mambo ya kutuaminisha Simba ni wakawaida hapa nchini usishangae haya ni mapenzi ya watu kwa timu nyingine ndo yanafanya waone kama Simba ni ya kawaida kisa tu kafungwa na Kagera au na Mbeya city, ni dhambi kubwa sana watu wanafanya kwenye hilo jambo,ukitaka kuamini Simba ni Dude kubwa nchini kwetu subiri msimu ujao tutakapopeleka timu nne michuano ya Afrika watakavokua wanafanya halafu utawatazama na Simba wanavofanya utaujua ukweli huu naosema, UKWELI.

Kibu Denis akipiga shuti mbele ya walinzi wa Orlando Pirates

Ukweli ni kwamba Kikosi cha Simba kwa sasa kimataifa hadhi yake ni makundi wakijitahidi sana ni Robo fainali lakini si zaidi ya hapo, na huu ndo ukweli halisi ulivo kabla ya kitu chochote.

Ukitoa bahati,  kujua (to be the best) lakini mpira unatabia ya kubaki kwenye ukweli na hapo ndipo watu wengi huwa tunashindwa kuzisukuma nafsi zetu kukubaliana na ukweli na tunabaki na mapenzi yetu hata kama yanatupotosha na kuuacha ukweli uende zake,
Umemfikiria Luis Miquissone ??umemfikiria Clotaus Chama?? umemfikiria Okwi?? unawafikiria lakini?? nauliza umewafikiria hao watu,je? ni team gani Tanzania wachezaji hao watakaa benchi?? huyo Okwi tunaeona amezeeka akirudi hapa nchini hawezi cheza BIG 4 yetu?? lakini ukweli unatuambia viwango vya wachezaji hao vinatosha kutufikisha Robo fainali hapo ni mpaka nguvu ya mwisho itatumika lakini si wachezaji wa kutupeleka nusu fainali na fainali achilia mbali kutupa makombe. 

Emmanul Okwi

Tazama Mwanakandanda timu ya ligi daraja la kwanza ya Tanzania (Championship) inapanda daraja kucheza ligi kuu ikifika ligi kuu inaachana na wachezaji wake walioipandisha daraja wanachukua wachezaji wa ligi kuu kwa mkopo toka kwa team kubwa na kusajili kwa wale ambao wanaona wanafaa ambao team zao zimeshuka daraja, unafikiri hawawapendi wale wachezaji waliotoka nao chini?? UKWELI ni kwamba level zao ni huko sio huku ligi kuu na huo ndo ukweli ambao tunatakiwa kuufahamu, ni ukweli unaouma.

Ukweli ni kwamba wakati Simba inawategemea akina Chanongo, Isihaka, Ndemla na Eddo ilikua inafanya hivo kulinda timu isishuke daraja lakini sio kubeba ubingwa au kushiriki kimataifa ndo maana sishangai kuwa simba wamewahi kushika nafasi ya nne ligi kuu mwaka 2013/14 sababu kikosi chao uwezo wao uliishia hapo. Walipoanza kusajili wachezaji wazuri wakarudi katika ushindani bahati mbaya wakipishana na Yanga nao wakaanza kuwategemea akina Deus Kaseka, Ukweli ni kwamba Kaseke anaweza kukupeleka michuano ya CAF lakini hatua ya awali tu mkatolewa uwezo wake umeishia pale ndio maana alipokua Singinda united alikua mchezaji wa kutegemewa huo ndio Ukweli.

Said Hamis Ndemla.

Baada ya hiyo mifano ya KWELI naomba nikwambie ukweli msioutaka, Luis Miquissone anacheza mechi zisizo na pressure kule Misri ukweli ni kwamba uwezo wake umeishia pale

Lakini anapokuja huku na kua ndio mchezaji wako tegemezi anawezaje kukupeleka Fainali kama hatua za makundi hachezi akiwa na Al Ahly?. Ukweli ni kwamba anahitajia kucheza pale level zake zilipo.

Luis Miquisone.

Ukweli ni kwamba timu unazoziona zinatamba Afrika hawatambi kwa bahati kama mnavotaka ukweli ni kwamba wamewekeza, wana wachezaji bora wengi wenye quality bora, ili nusu fainali iwe sehemu ya maisha yako unatakiwa angalau uwe na wachezaji wa viwango vya juu yaani juu kabisa Afrika wawe kuanzia saba, angalau nusu fainali kwako utaweza kuinusa.

Kupitia huu ukweli nataka kusema  kwamba Simba simuoni akivuka Robo fainali dhidi ya Orlando Pirates.  Kwenda nusu fainali kwa quality, kitu pekee kitakachowapeleka Simba nusu fainali ni BAHATI tu, unaijua bahati?
Ni kama Villareal kumfunga Bayern. Sasa bahati (Fluk) haiwi kila siku hutokea tu kama ajali ndo maana unaona team imezidiwa kila kitu na wapinzani wake kuanzia dakika 1-90 ila yule mbovu akashinda. 

Al-Ahly mabingwa mara mbili mfululizo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Asante Simba kwa kutuheshimisha Tanzania, ukweli ni kwamba sajilini wachezaji wa Nusu fainali hao mlio nao hawawezi kuwapeleka nusu fainali hata mcheze hivyo miaka 100 kama tulivokua tunahangaika kufika mtoano miaka nenda rudi hadi dawa ilipopatikana.

Celestine Chomola.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.