Mosses Phiri "Jenerali"
Tetesi

Uongozi Simba: Moses Phiri Haendi Kokote

Sambaza....

Kumekuwepo na tetesi kuelekea usajili utakaoanza mwezi ujao mshambuliaji wa Simba Moses Phiri huenda akaachana na Simba kutokana na kukosa furaha kikosini humo akikosa nafasi ya kucheza mbele ya Mcongomani Jean Baleke. 

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameonekana kukanusha kuondoka kwa Moses Phiri “General” mwenye mabao 10 mpaka sasa katika Ligi Kuu ya NBC. Phiri ambae alianza msimu vyema kabla yakupata majeraha na kupelekea kupoteza fomu yake ya ufungaji.

“Majeraha msimu huu yamemkatili General asiwe mfungaji bora wa CAF Champions League, asiwe mfungaji bora wa Tanzania, asiwe mchezaji bora wa Tanzania,” alisema Ahmed Ally kupita ukurasa wake na instagram na kuongeza “Yote haya kwa Phiri yanawezekana kutokana na moto aliyonao nao na ubora aliyokua nao.”

Moses Phiri “katikati” akifunga mbele ya walinzi wa Nyassa Big Bullets.

Ahmed Ally anaamini nyota huyo wa Zambia akiwa timamu kabisa na atakua hakishikiki kwa maana hiyo akivunja tetesi na maneno yote yaliyosemwa kuhusu kutaka kuondoka kutokana na kukosa nafasi mbele ya Robertinho ambae kipenzi chake kikubwa ni Jean Baleke

“Tunaamini kipindi cha mapumziko ya ligi kitampa nafasi ya kupumzika na ku recover zaidi kwa ajili ya msimu ujao. Kitu pekee wana Simba tunasubiri kwa hamu ni kuona General anakua fit kwa asilimia mia moja. Wana Simba tunakuombea sana urudi kazini,” alimalizia Ahmed Ally.

Sambaza....