ASFC

Ushindi raha, kuifunga Yanga raha maradufu!

Sambaza kwa marafiki....

Klabu ya Yanga ilipoteza matumaini ya kuingia fainali ya kombe la shirikisho, na zaidi kupoteza matumaini ya kucheza mechi za kimataifa msimu ujao. Hii ni baada ya kupokea kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa wazee wa Kamwene maarufu toka enzi hizo, Wanapaluhengo, Lipuli Fc.

Magoli ya Lipuli yalifungwa na Paul Nonga na mshambuliaji aliyeitwa kwa mara kwanza katika kikosi cha Stars, Miraj Athumani.

Akiwa katika furaha ya kiwango cha juu Paul Nonga aliimbia Kandanda.co.tz “Hii ni mafanikio makubwa sana kwetu, na tumefanya vile mashabiki wapenzi wa mkoa wa Iringa walichotaka pamoja na kila mdau wa mpira mjini hapa”.

Nonga (kupia) na Miraj (Kushoto)  wakati wa Mazoezi

Tulipomuuliza vipi pia kuhusu ushindi huu ulioambatana na kuifunga Yanga “Ushindi raha, kuifunga Yanga raha maradufu! tena kwa kuifunga na kuingia Fainali! aahh rahaa sana” Nonga mwenye furaha alitujibu hivyo na kusisitiza “Yanga walikuwa bora, ila sisi tumekuwa bora zaidi yao leo (jana) sababu tumepata matokeo”.

Goli la Nonga

Ikumbukwe kuwa Nonga amewahi ichezea pia klabu ya Yanga.

Lipuli inaenda kwa kifua mbele mjini Lindi kwaajili ya fainali hiyo ambayo itaikutsnisha na Azam Fc kutoka jijini Dar es salaam.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.