Ligi Kuu

Saliboko awapa KMC mapumziko.

Sambaza....

Uongozi wa Timu ya KMC FC umetoa mapumziko ya siku 10 kwa wachezaji wake ambapo watapaswa kurejea kambini Machi 19 ili kujiandaa na michezo iliyobakia ya Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara ambapo Aprili 17 itakipiga dhidi ya Geita Gold katika Uwanja wa Uhuru hapa Jijini Dar es salaam.

Mapumziko hayo yamekuja kutokana na kwamba KMC FC haitakuwa na mchezo kwa mwezi Machi hadi Aprili 17 na hivyo kutoa nafasi kwa wachezaji wake kujipa muda wakujipanga vema kwenye michezo mitano iliyobakia kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2022/ 2023.

Daruwesh Saliboko.

Aidha Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana imecheza mchezo wake wa 25 jana dhidi ya Kagera Sugar na kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa sifuri ambayo yalifungwa na Daruweshi Saliboko na hivyo kuvuna alama zote tatu muhimu na kupanda kwa nafasi moja juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Christina Mwagala “Tumewapa wachezaji wetu mapumziko ya siku 10 ili waende wakajiandae vema kumaliza msimu, tulipita kwenye kipindi kigumu ambacho hatukuwa na matokeo rafiki na hivyo jana kupata ushindi ambao umetupa morali ya kujipanga upya tutakaporejea.” 

“Ukiangalia Ligi ni ngumu na Timu zote zilizopo hivi sasa kila mmoja anataka kupata matokeo jambo ambalo ni zuri hivyo kama Timu ya Manispaa ya Kinondoni tutarudi tukiwa na nguvu, hari na morali nzuri na kumaliza msimu tukiwa kwenye nafasi nzuri,” Mwagala aliongeza

KMC FC itakaporejea mbali na kukutana na Geita Gold Aprili 17 , pia itakuwa na kibarua kingine dhidi ya Dodoma Jiji, Singida Bigi stars, Tanzania Prisons pamoja na Mbeya City ambapo kati ya hizo mbili zitachezwa nyumbani huku tatu zikipigwa ugenini.


Sambaza....