Blog

Vipaji vikubwa vya Kandanda Duniani hutokea Afrika!

Sambaza....

Unapoitaja Cameroon kwa maana ya timu ya Taifa ni sawa kabisa na umetamka ‘Indomitable Lions’ au Simba walioshindikana

Unapotamka Taifa hilo la Cameroon inataja mrundikano wa vipaji vikubwa toka vilivyosumbua katika kombe la Dunia hasa mwaka 1990 kule Italia.

Roger Milla.

Binafsi nikiwa naanza kupata ufahamu wa soka huyu mwanaume pichani Roger Milla ndiyo alikuwa star mkubwa wa Taifa hilo nadhani ilichangiwa na Super Performance yake ya World Cup 1990 alipomaliza na goli nne akiwa na umri mkubwa kisoka kwa maana 38.

Lakini alama pekee aliyoiacha kwenye mashindano hayo ilikuwa ni aina ya ushangiliaji wake kwa lugha nyingine waweza kusema ndiyo muasisi wa kushangilia kwenye kibendera( Roger Milla dance)huku akikata viuno ,

Roger Milla akishangilia kwenye kibendera “Roger milla dance”.

Nyakati hizo ushangiliaji maarufu wa washambuliaji wa zamani ilikuwa’ kuruka juu na kupiga ngumi hewani’ huku vikitamkwa baadhi ya maneno.

Mzee Roger alianzisha style hii ambayo hadi wakati huu sijui kama aliipanga kufanya vile au ilikuja automatically

World Cup ya 1990 Mzee huyu alikuwa na umri wa miaka 38 na kama akavunja rekodi ya kuwa mchezaji mkubwa ki umri kufunga goli kwenye kombe la dunia na watafiti wa mambo wanasema kama angekuwa mkweli juu ya umri wake sahihi huwenda hiyo rekodi ingevutia zaidi

Roger Milla akimtambuka mtu katika moja ya mchezo wa Kombe la Dunia.

Wakati wengi wakiamini World Cup ya 1994 si zama zake tena ,Mzee huyu alikuwepo Marekani na alifunga tena katika mchezo ambao Cameroon walifungwa mabao 6 – 1 na Russia mind you wakati huo alikuwa na miaka 42

Nachotaka kusema ni kweli vipaji vikubwa top talent au abnormal talent za Africa nyakati hizi zinatoweka kabisa wapo wachezaji wengi wazuri lakini kufikia uwezo wa wachezaji wa zamani ni shughuli pevu wakati nawaangalia game ya Burundi na Cameroon sioni material ya wachezaji hawa au akina Patrick Mboma Alphonce Tchami ,Raymond Kala Emanuel Kunde, Biyiki Brothers Makanaki Luis Mfede.

Vicent Aboubacar.

Hata nusu ya talent ya Samuel Eto ambaye alikuwepo uwanjani pia sikuona huwezi kuniambi Toko Ekambi Erik Chaupo Moting au Vincent Aboubakar anaweza kukupa nusu ya uwezo wa Fills.

Vipaji vyao vikubwa vilimfanya gwiji Pepe Kalle kuwaimba hawa jamaa na kuwasifia mno

Sambaza....