BlogLigi Kuu

Waamuzi waliwaua Alliance Fc dhidi ya Yanga

Sambaza....

Jana kulikuwa na mechi kati ya Alliance Fc na Yanga uliokuwa unachezwa katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Baada ya mchezo huo, Kandanda.co.tz ilimtafuta msemaji wa klabu ya Alliance Fc, Jackson Mwafulango.

Msemaji huyo amedai kuwa kwa kiasi kikubwa Mwamuzi amechangia matokeo hayo ya wao kufungwa.

“lakini kikubwa niseme kuwa kwamba, Mimi napenda waamuzi wawe wanaangalia, tumenyima takribani penalti tatu”.

” Lakini mwisho wa siku mpira wa miguu uko hivo, na haya ndiyo matokeo ya mpira wa miguu ingawa tumenyima penalti tatu”. Alisema msemaji huyo.

Alliance FC wamepoteza mechi yao ya 11 kwenye ligi kuu. Baada ya mechi hii, Alliance ataenda kucheza na Coastal Union jijini Tanga.

Alliance FC wamepoteza mechi tatu kwenye uwanja wa CCM Kirumba, walipoteza mechi dhidi ya Mbao Fc, Azam Fc na Yanga. Lakini hawajawahi kupoteza mechi katika uwanja wa Nyamagana.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.