Shirikisho Afrika

Yanga Bado Wananafasi, Mayele Ameanzisha Vita Nyingine kwa Yanga

Sambaza....

Wapwa, binafsi bado na matumaini matokeo kitu kingine “performance” ni kitu kingine Wananchi ni washindani lolote linaweza kutokea mkondo wa pili.

Makosa madogo madogo ya kiufundi yakifanyiwa kazi na maandalizi ya kucheza kwenye hali kama ya leo (hali ya mvua). Sijui kama umegundua hali ya hewa na utelezi fulani haukuwa rafiki ikimaanisha viatu maalum vilipaswa kutumika. 

Pia Wapwa Kiukweli Fiston Mayele ni mwamba ameng’aa sana kwenye michuano hii ya CAF goli alizofunga 13 (tangu hatua ya awali ya Ligi ya mabingwa) zinatosha sana kumtambulisha kimataifa zaidi.

Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto akiruka juu na mshambuliaji wa USM Algiers Ahmed Mahiuos.

Naona Wananchi kwenye vita vingine baada ya fainali ya kupambana kumbakiza tunaposema mpira si mchezo wa siri kama unajua unajua tu na utaonekana hadharani huwa tuna maana kama hii.

Nimeona magoli yake mengi tangu amekuja nchini lakini goli la dhidi USMA ni bora sana, upokeaji wake wa mpira, na jinsi alivyochagua eneo la kupiga na mpira ulipokwenda kwa maana ya zao “fantastic” kabisa. 

Yanga sasa wanakibarua chakupindua matokeo ugenini ambapo wanapaswa kufunga mabao mawili kwa sifuri ili kuweza kutwaa ubingwa. Wapwa mimi binafsi kiufundi nakubaliana na hilo na bado naendelea kusimama na Mayele katika mchezo huo. Kila lakheri Wananchi.

Sambaza....