Tetesi

Yanga kumtambulisha kocha wake mzawa!

Sambaza....

Kocha mkongwe Juma Mwambusi yuko njiani kuelekea kutambulishwa kama kocha msaidizi wa klabu ya Yanga ambapo atakwenda kufanya kazi na kocha mkuu raia wa Burundi.

Mwambusi msimu uliopita alikua akihudumu kama kocha mkuu wa Mbeya city kabla ya kutupiwa virago itakua si mara yake ya kwanza kufanya kazi na Wanajangwani hao. Ikumbukwe Mwambusi alihudumu Yanga kama kocha msaidizi chini ya Hans Plujim.

Benchi la ufundi la Yanga litakua chini ya Cedrik Kaze (Kocha Mkuu), Juma Mwambusi (Kocha Msaidizi), Vladmir Niyonkuru (Kocha wa makipa) na Hafidh Saleh (Meneja).

Utambulisho wa benchi jipya la ufundu unatarajiwa kufanyika hivi karibuni kabla ya kufikia lilele cha siku ya Mwananchi Jumapili August 30.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.