AFCON

Yanga watoa washambuliaji, Simba wao ni viungo tu.

Sambaza....

Kocha wa Timu ya Taifa ya Zambia “Chipolopolo” Avram Grant ametaja kikosi cha wachezaji 27 watakaounda kikosi kitakachocheza na Lethoto katika michezo miwili yakufuzu Afcon.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea amejumuisha nyota wanaocheza nje na ndani ya Bara la Afrika ili kuunda kikosi chake hicho chenye matumaini makubwa yakufuzu  michuano hiyo ya Afcon.

Katika kikosi hicho wamejumuishwa washambuliaji wawili nyota walipishana Jangwani katika kipindi cha dirisha dogo. Grants amemjumuisha mshambuliaji wa Yanga Kenedy Musonda lakini pia Lazarious Kambole wa Zesco United.

Clatous Chama.

Kambole aliyekua mchezaji wa Yanga kabla ya kumtoa kwa mkopo dirisha hili dogo kwenda Zesco United amekua na wakati mzuri tangu ajiunge nao na hivyo kumfanya kocha hiyo wa Chipolopolo kumjuisha licha ya majeruhi yaliyomuandama na kumfanya kushindwa kuitumikia Yanga.

Pia katika kikosi hicho amejumuishwa kiungo wa Simba Clatous Chama na pia kiungo wa Amazulu Rally Bwalya aliyekua mchezaji wa zamani wa Simba.


Sambaza....