Tetesi

Yanga yamalizana na AS Vita kuanza kushusha Wacongo

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga inaendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao kwa kuendelea kufanya usajili wa kikosi chake na sasa wamehamia katika usajili wa Kimataifa.

Yanga kupitia wadhamini wao GSM wamekamilisha usajili wa nyota wawili wa AS Vita na huenda wakawatangaza wakati wowote kuanzia leo hii kama wachezaji wao wapya watakaowatumia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Baada ya Eng. Hesri kuonekana katika picha ya pamoja na viongozi wa AS Vita pamoja na kocha Florentine Ibenge mashabiki wa Yanga walikua wana hamu ya kujua kama ni kweli timu yao imemalizana na kocha Ibenge kama ambavyo inavyotajwa.

Yanga imeshamalizana na kiungo Mukoko Tonombe ambae anakwenda kuchukua nafasi ya Mcongo mwenzie pia Papy Tshishimbi ambae ameshindwa kuelewana na uongozi kwenye maswala ya mkataba

Mukoko Tonombe

Mchezaji wa pili ni Tuisila Kisinda ambae anacheza kiungo mshambuliaji wa pembeni ambae pia Yanga wamemsajili ili kuongeza kasi eneo la pembeni lakini pia uzoefu katika kikosi chao hicho ambacho kinaundwa upya baada ya msimu uliomalizika kufanya vibaya.

Baada ya baadhi ya nchi kuanza kufunga anga zao tayari Yanga sc imeshaanza na kunufaika na urejeo wa safari za Kimataifa za ndege kwa kuendelea kumalizana na wachezaji ambao walikua wanawahitaji.

Tuisila Kisinda.

Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji wa ndani Yassin Mustapha, Kibwana Shomari, Bakari Mwamunyeto, Zawadi Mauya, Abdalah Shaibu, Farid Mussa, Waziri Junior.

Sambaza....