Ligi Kuu

Yanga yapelekwa Kigoma!

Sambaza....

Uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting umethibitisha nchezo wao wa mzunguko wa pili dhidi ya Yanga hautapingwa Mwanza CCM Kirumba wala Dar es Salaam kwa Mkapa.

Kupitia msemaji wao Masau Bwire wamethubitisha kuwapeleka Wananchi mkoani Kigoma katika dimba la Lake Tanganyika.  Uwanja huo ulitumika katika mchezo wa Fainali ya FA msimu uliomalizika ambapo Simba aliibuka na ushindi wa bao moja bila.

Feisal Salum akimtoka Zuberi Dabi.

“Tuna mechi dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Ilulu hapo tukimalizana nao tarehe 18 tunajiandaa kupambana nao hapo tutakutana na Yanga.

Tunawapeleka kwenye uwanja ambao tumeutafakari kwa muda, (Lake Tangayika) kwa mujibu wa kanuni ya 9 kifungu kidogo cha 7 kinaturuhusu kuwapeleka uwanja mwingine na hilo inatupasa tufanye ndani ya siku 21.”


Ruvu Shooting watakutana na Yanga katika mchezo wa NBC Premier League May 4 mwaka huu katika mzungungo wa pili wa Ligi ambapo katika mzungungko wa kwanza Yanga walishinda mabao matatu kwa moja katika uwanja wa Benjamin Mkapa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.