Sambaza....

Timu ya Yanga imefanikiwa kushinda katika uwanja wa sokoine mkoani Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons

Tanzania Prisons walikuwa wa kwanza kufunga goli, kabla ya Ibrahim Ajib kusawazisha goli hilo.

Amis Tambwe aliyetokea benchi aliiwezesha Yanga kufunga goli la pili. Wakati mpira ukiwa unaelekea mwishoni , Amis Tambwe tena alifunga goli la tatu na goli lake la nne msimu huu katika mechi 3 alizocheza.

Yanga ambayo ilikuwa na ratiba ya mechi nyingi katika uwanja wa Taifa ilikuwa inatazamiwa kupata matokeo mabaya katika viwanja vya mikoani.

Lakini mpaka sasa Yanga imefanikiwa kujikusanyia alama Tisa katika michezo mitatu ya mikoani. Yanga ilishinda dhidi ya Mwadui mkoani shinyanga, ikashinda dhidi ya Kagera sugar mkoani Kagera na Leo hii imeshinda dhidi ya Tanzania Prisons mkoani Mbeya.

Sambaza....