Ligi Kuu

Yanga yatangaza kutumia uwanja mpya.

Sambaza....

Kufuatia kufungiwa kwa uwanja wa Benjamin Mkapa kwa michezo ya ndani imewalazimu kutafuta uwanja mwingine ambao wataumia katika michezo ya FA na Ligi Kuu ya Championship.

Alli Kamwe msemaji wa Yanga amethibitisha klabu yao itatuamia uwanja wa Azam Complex uliopo Chamanzi katika mchezo wao ujao wa FA dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Alli Kamwe “Mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons katika michuano ya FA tutatumia uwanja wa Azam Complex pale Chamanzi na hii ni kutokana na uwanja wa Mkapa kufungiwa kwa michezo ya ndani.”

Yanga watawaalika Prisons katika mchezo wa raundi ya nne ya Azamsports Federation Cup siku ya March tatu katika muendelezo wa michuano hiyo.

Shirikisho la soka Barani Afrika CAF limeufungia uwanja wa Mkapa ambao unatumiwa na vilabu vya Simba na Yanga kama uwanja wao wa nyumbani ili uweze kufanyiwa marekebisho madogo na pia kutunza sehemu yake ya kuchezea “pitch”.

Na hii inapelekea Yanga kutafuta uwanja mwingine watakaoutumia kwa michezo yao ya Ligi. Kwa Jiji la Dar es salaam Yanga walikua na machaguo mawili Uwanja wa Uhuru au Azam Complex lakini Alli Kamwe tayari ametangaza rasmi uwanja watakaoutumi.

“Yanga tutatumia uwanja wa Azam Complex katika michezo yetu ya Ligi iliyobaki kama uwanja wa Taifa kufungiwa kwa muda.” Alisema Alli Kamwe.

Katika mwezi huu Yanga ina michezo mwili pekee watakayocheza nyumbani katika michuano ya ndani dhidi ya Prisons March tatu na dhidi ya Geita Gold  March 12.

Sambaza....