Blog

Yupi kocha bora 2019 kati ya Aussems na Zahera?

Sambaza....

Tukiwa tunaelekea mwisho wa mwaka 2019 , ingia ndani ya kandanda.co.tz andika kura yako kwenye tovuti na mshindi atapewa tunzo na Kandanda.co.tz

Ettiene Ndayiragije

Ettiene kwa sasa anaifundisha timu ya Taifa ya Tanzania, mwaka 2019 aliiwezesha klabu yake ya KMC kwa mara ya kwanza kucheza kombe la shirikisho Afrika, pia ilimaliza katika nafasi ya nne Ligi Kuu Msimu wa 2018/19. Alijiunga na Azam Fc kabla ya kuteuliwa kuiongoza timu ya taifa.

Mwinyi Zahera

Zahera moja ya makocha waongeaji sana kuwahi kutokea katika Ligi Kuu, mafanikio makubwa aliyoyapats na Yanga ni kushiriki klabu Bingwa Afrika na Shirikisho Afrika. Aliiongoza Yanga kumaliza katika nafasi ya pili Ligi Kuu Msimu 2018/19.

Patrick Aussems

Kupitia Aussems, klabu ya Simba kwa mara ya kwanza ilifanikiwa kufika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika, pia na kufanikiwa kutetea taji lake la Ligi Kuu 2018/19. Zahera alisitishiwa mkataba wake baada ya kushindwa kufikia malengo waliyokubaliana na klabu yake.

Selemani Moja

Moja ya mafanikio makubwa ya klabu ya Lipuli Fc mwaka huu ni kufanikiwa kuingia katika fainali za kombe la shirikisho la azam (ASFC), ikiwa ni mara yao ya kwanza ingawa hawakufanikiwa kuchukua. Lipuli ilikuwa na mwaka mzuri na matokeo mazuri ikimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi 2018/19.


YUPI KOCHA WAKO BORA ZAIDI KWA MWAKA 2019? Tuandikie….

Kocha wa Mwaka

  • Patrick Aussems (Simba Sc*) (67%, 6 Votes)
  • Mwinyi Zahera (Yanga Sc*) (22%, 2 Votes)
  • Selemani Moja (Lipuli Fc*) (11%, 1 Votes)
  • Ettiene Ndayiragije (KMC Fc*) (0%, 0 Votes)

Jumla ya Kura: 9

Loading ... Loading ...


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.