Zlatan Ibrahimovic akiagana na mashabiki wa AC Milan.
Stori

Zlatana Ibrahimovic Atundika Daruga Akiwa na AC Milan

Sambaza....

Nguli wa soka Zlatan Ibrahimovic ametanga kustaafu soka rasmi akiwa na AC Milan ya nchini Italy akiwa na umri wa miaka 41. Tayari Zlatan alishatangaza hatoongeza mkataba tena na Milan baada ya kurudi kuitumikia kwa kipindi cha pili.

Zlatan na Milan walitumia mchezo wa Seria A dhidi Verona kuagana ambapo katika mchezo huo wachezaji wenzake walimuwekea “Guard of honour” nyota huyo kutoka Sweden. Katika mchezo huo Milan iliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Akizungumza katika mchezo akitangaza kustaafu kwake Zlatan Ibrahimovic amesema “Nataka kuishukuru familia yangu, kila mtu wa karibu kwangu kwa uvumilivu wao, nataka kuwashukuru familia yangu ya pili, wachezaji. Napenda kuwashukuru (Kocha Mkuu wa AC Milan, Stefano) Pioli na wafanyakazi wake kwa jukumu ambalo mmenipa. Ninataka kuwashukuru wasimamizi kwa nafasi hiyo.”

Zlatan Ibrahimovic akiagwa na wachezaji wenzake wa AC Milan.

“Lakini zaidi ya yote: kutoka moyoni mwangu nataka kuwashukuru nyinyi mashabiki. Mlinipokea kwa mikono miwili, mlinifanya nijisikie nyumbani. Nitakuwa shabiki wa Milan maishani. Wakati umefika wa kuaga soka, lakini si kwako mshabiki wa Milan”

Ibrahimovic ambae alishinda taji la Seria A na AC Milan mwaka 2011 na pia msimu uliopita aliisaidia tena Milan kubeba taji hilo ikiwa baada ya muda mrefu kutwaliwa na Juventus.

“Nina hisia nyingi sana zinazonipitia. Tuonane karibu, ikiwa una bahati. Forza Milan na kwaheri,” alimalizia Zlatan.

Kwaheri Zlatan

Zlatan alijiunga mara ya pili na Milan mapema mwaka 2020 lakini majeruhi ya mara kwa mara yakamfanya kushindwa kuonyesha makali yake na kufunga magoli 34 pekee.

Mfungaji bora huyo wa muda wote wa Sweden akiwa na mabao 62 kwenye michezo 121 alipokea jumbe nyingi za kumuaga na kumtakia kila lakheri katika maisha yake mengine.

Ukurasa rasmi wa AC Milan uliandika “Zama zinakwisha, manguli wanaishi milele.”, pia wakaongeza “milele miongoni mwetu” na kisha wakamalizia “humwinamii mfalme yeyote yule.”

Zlatan Ibrahimovic akiitumikia Manchester United alifanikiwa kuwapa taji la Europa League na Kombe la Carabao.

Zlatan alianza kuonekana na Malmo ya kwao Sweden mwaka 1999 kisha akahamia Ajax ya Uholanzi na ndipo alipoanza kuteka dunia kwa magoli yake na kipaji chake kikubwa kikazidi kuonekana.

Mwaka 2004 mpaka 2006 akahamia Juventus na kuifungia mabao 23, kisha akatimkia Inter Milan akiifungia mabao 57 katika michezo 88 na kuondoka zake Italy.

Si Italy tuu Zlatan akahamia Hispania Barcelona lakini hakuwa na wakati mzuri kule kutokana na kutokua na mahusiano mazuri na Pep Guardiola. 

Zlatan Ibrahimovic akiwa Inter Milan.

Baada ya hapo akarejea Milan akikaa kwa misimu miwili kisha akatimkia PSG akicheza michezo 122 akifunga mabao 113, halafu akaenda EPL akiwa na United akifunga mabao 17 katika michezo 33 na kwenda Amerika akitumikia LA Galaxy na baadae akarejea Milan kwa mara nyingine.

Huyo ndio Zlatan Ibrahimovi mchezaji mjivuni na jeuri haswa huku akiamini katika kipaji chake na umaridadi wake akiwa uwanjani. 

Sambaza....