Sambaza....

IMASSIMILIANO Allegri ameunganishwa katika orodha ya makocha ambao wanahitajika kuchukua nafasi ya Arsene Wenger, pindi atakapo achana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu

Juventus ina karibia kushinda Scudetto kwa msimu wa saba mfululizo, na ikimuacha Napoli nyuma ya pointi sita. Lakini uvumi ambao unaendelea unasema kwamba Allegri anaweza kuondoka mwisho wa msimu huu

Allegri na Luis Enrique, wanatajwa kuwa makocha sahihi ambao wanaweza kuifanikisha Arsenal, ambapo wanapo ondokewa na kocha Wenger aliyedumu na klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi

Hata hivyo, mtendaji mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta, alisikika akisema kwamba bado wana nafasi kuendelea kumshawishi Allegri kuendelea kubaki na Juventus

“Sisi na Allegri tuna uhusiano mzuri baada ya kufanya naye kazi vizuri, hivyo tutatumia nafasi ya kuendelea kumbakiza hapa

“Baada ya kushinda Scudetto tutazungumza nae juu ya siku zijazo ndani ya klabu hii, ambapo nina uhakika kuwa ataridhika pamoja nasi,” alisema Marotta.

Sambaza....